Tanzania ni nchi yenye mazingira mazuri na ya kuvutia, mbuga nzuri zenye wanyama na ndege wa kila aina- ambazo kwa muda mrefu zimekuwa kivutio kikuu kwa watalii. Ukichunguza kwa undani utagundua kuwa, mazingira/maliasili ya nchi yetu ndio inatupatia heshima kubwa watanzania-kuanzaia mlima Kilimanjaro, Mbuga mbali mbali zijulikanazo duniani kote, Maziwa na mito mikubwa mpaka katika majina ya viburudisho kama Kilimanjaro, Ndovu na Serengeti- yote katika kutangaza mazingira ya mtanzania.
"Kwa ujumla, mazingira ni muhumu sana kwani yanaipatia nchi mahitaji yote ya msingi kwa ajili ya kufanikisha masuala ya jamii na uchumi. Mazingira ndiyo makazi ya viumbe vyote – mimea na wanyama ambao ndiyo urithi usiokuwa na badala yake. Mazingira ni chombo cha kuweka yale yasiyofaa. Mazingira ni msingi ambao ndiyo itakuwa jawabu la kupunguza unyonge wa umaskini." Pia, sekta ya maliasili, mazingira na utalii inachangia zaidi ya 14% ya bajeti ya Tanzania.
Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ( ambayo kwa kiasi kikubwa yanatokana na athari za shughuli za mwanadamu), hari ya uoto halisi/ asili wa mazingira umeanza kutoweka na kuathili baadhi ya maeneo hapa nchini Tanzania. Serikali ya Tanzania ilitambua hatari ya kupoteza rasilimali hiyo kama vile hewa safi, mabaki ya mimea na wanyama wa kale, nyangumi, miti ya asili na wanyama/mimea ambayo iko mbioni kutoweka.
Pamoja na serikari kuhusika moja kwa moja katika kutunga sera za mazingira, bado wananchi tunalo jukumu la kulinda hali hii ya uharibifu isiendelee kuwepo na hatimaye kuharibu mazingira. Serikari inatakiwa kuweka msukumo mkubwa wa uongozi wa mazingira ili kulinda sehemu asili ya kuishi binadamu na kuoanisha upungufu uliopo kwenye mazingira katika kusaidia kufikia maamuzi yanayohusu masuala na shughuli za uchuminikiwa ni pamoja na kutengeneza sera, sheria na mfumo wa taratibu ambazo zinaendana na masuala ya jamii, uchumi na siasa.
Pia, taasisi za serikari na zisizo za serikari zijikite katika kutoa elimu juu ya umuhimu wa mazingira, elimu ambayo itaendeleza ujuzi ambao utasaidia katika kuhifadhi na kuendesha masuala ya mazingira kwa manufaa yao na manufaa ya vizazi vijavyo.
Vyombo vya habari (radio, televisheni, magazeti) pia vizidi kuhamasisha na kutangaza vipindi mbalimbali vya elimu kuhusu masuala ya mazingira ili kutoa mafunzo kwa hadhara na watu binafsi ya kuwa na moyo wa kupenda, kujituma na kufahamu jinsi ya kuhifadhi na kusimamia mazingira.
Kwa kufanya hivyo, jamii na serikari kwa ujumla itakuwa imesaidia kwa kiasi kikubwa kulinda maliasili na maingira hivyo itasaidia kushinda matatizo yanayotokana na umaskini, maradhi, hali mbaya na duni ya upatikanaji wa chakula, makazi machafu, maji yasiyo salama, upatikananji wa nishati usioridhisha na ukosefu wa ajira.
Did you miss the making of my show in Serengeti?
Click here to subscribe and watch my shows on YouTube.
No comments:
Post a Comment